August 2026
%AutoEntityLabel: 704d1890-e482-4fa8-971d-7d23fd3adbc5%
%AutoEntityLabel: 98ff23ea-f376-4079-a9ea-0540f67162cb%
Isaya 32:1-4 - 14-08-2026
Amosi 5:6-8 - 13-08-2026
Mathayo 5:14-16 - 12-08-2026
2 Petro 1:3-11 - 08-08-2026
Luka 10:38-42 - 06-08-2026
Council of Elders 2026 -2030
Council of Elders | Wazee wa Kanisa 2026 -2030
Ufunuo wa Yohana 2:8-11 - 05-08-2026
Matangazo ya usharika Tarehe 2 Agosti 2026
DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 02 AGOSTI, 2026
SIKU YA BWANA YA 9 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA NI:
“MWENENDO WENU UWE WA HEKIMA”
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni:hakuna mgeni aliyetufikia na cheti: Kama kuna wageni ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki nasi wasimame ili tuwakaribishe.
3. Matoleo ya Tarehe 26/07/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
Waefeso 4:17-19 - 04-08-2026
RASMI: Safu Mpya ya Baraza la Wazee Azania Front Yaanza Kazi 🙏
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Baba Askofu Dkt. Alex Malasusa amewabariki na kuwaingiza kazini rasmi wajumbe wapya wa Baraza la Wazee wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front katika ibada iliyofanyika Usharikani hapo, siku ya Jumapili, 2 Agosti 2026.
Safu hiyo mpya ya Baraza la Wazee ilipatikana katika mchakato wa uchaguzi uliofanyika katika Usharika wa Azania Front siku ya Jumapili, 14 Juni 2026 na itauongoza usharika kwa kipindi cha miaka minne (2026-2030).
PICHA: Maendeleo ya Ujenzi wa Nyumba za Wageni, Kituo cha Kiroho Kiharaka
Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front, Chaplain Victor Makundi amewashukuru washarika kwa kuendelea kutoa michango yao ili kukamilisha ujenzi wa nyumba za wageni unaoendelea katika Kituo cha Kiroho Kiharaka, Bagamoyo mkoani Pwani.
Akitoa tathimini na mwelekeo wa ujenzi wa nyumba hizo katika ibada ya Jumapili, 2 Agosti 2026, Usharikani Azania Front, Chaplain Makundi amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika mwaka 2028, hivyo amewaomba washarika kuendelea kutoa michango yao ili lengo la kukamilisha mradi huo kwa wakati liweze kutimia.
