Matangazo ya usharika ya tarehe 13 Septemba 2026

DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI MATANGAZO YA USHARIKA  TAREHE 13 SEPTEMBA, 2026 SIKU YA BWANA YA 15 BAADA YA UTATU, NENO LINALOTUONGOZA NI:  

“MUNGU HUJISHUGHULISHA NA MAMBO YETU”

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti:

3. Matoleo ya Tarehe 30/08/2026

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

- Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONTCATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 06/09/2026 ni Washarika 760 na Sunday School  272

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia wazazi na walezi kuwa mazoezi Ya mikaeli na watoto yanaendelea kila Jumamosi.  Muda, kwa ibada ya kingereza ni saa 3:00 hadi saa 6:00 mchana, na ibada ya Kiswahili ni saa 6:00 hadi saa 8:00 mchana.  

8. Kutakuwa na Ibada maalum ya Wajane na Wagane Kijimbo itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 20.09.2026 kuanzia saa 8:00 mchana katika Usharika wa Kipawa.Ibada hii itaongozwa na Mkuu wa Jimbo na itaambatana na Sakramenti ya meza ya Bwana.

9. Kwaya ya Umoja inaendelea na mazoezi ya Reformation kila Jumanne na Jumatano  saa 11:00 jioni. Wanakwaya wote mnaombwa kuhudhuria bila kukosa na kwa wakati.

10. Vitabu vya Ibada ya nyumba kwa nyumba vinapatikana  dukani.

11. Leo tutatoa sadaka ya Msamaria Mwema. Sadaka hii ni kwa ajili ya kusaidia vituo vyetu vya Diakonia.

12. Shukrani  

13. NDOA. Ndoa za Washarika Hakuna ndoa ya Msharika

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

14. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

 

- Mjini kati: Itafanyika Kanisani siku ya Jumamosi saa 1:00 kamili asubuhi.

Tegeta,Kunduchi,BahariBeach,Ununio,Boko:Kwa .Bw& Eng Eng Lema  

- Oysterbay na Masaki: Kwa Abdiel Mengi

- Upanga: Kwa Bw & Bi Mbwilo

- Madale, Goba, Mivumoni: kwa  Bw & Bi Godfrey Moshi

 

15. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya azaniafront. or.tz, pia tuna kurasa Facebook na Instagram.

16. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki