Alhamisi asubuhi tarehe 13.08.2026;
Amosi 5:6-8
6 Mtafuteni Bwana, nanyi mtaishi; asije akawaka kama moto katika nyumba ya Yusufu, nao ukateketeza, asiwepo mtu awezaye kuuzima katika Betheli.
7 Ninyi mnaogeuza hukumu kuwa uchungu, na kuiangusha haki chini,
8 mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza kwa usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; Bwana, ndilo jina lake;
Haki huleta amani na ustawi;
Nabii Amosi anaimba wimbo wa huzuni kwa ajili ya ufalme wa Israeli ya Kaskazini akisema Taifa limeanguka na haliwezi kuwepo tena. Mungu anaonya kwamba anguko kubwa linakuja akimaanisha kwamba wengi watakufa au watakuwa mateka. Mungu anawataka watu kuacha kutafuta msaada kwa viongozi wala rushwa, bali kumtazama yeye.
Somo linaonesha Amosi akiwaambia kumtafuta Bwana ndipo wataishi. Ndiyo wito tunaopewa asubuhi ya leo, kumtafuta Bwana ili tukaishi. Yaani tunapewa wito wa kudumu katika imani ili tuufikie uzima wa milele tulioahidiwa na Kristo aliyetuita. Mwamini sasa uokolewe. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
Butainamwa/Bukoba
