Date
Reading
Warumi 10:1-4

Jumatatu asubuhi tarehe 05.10.2026;
Warumi 10:1-4
1 Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe.
2 Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.
3 Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.
4 Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.
Uhuru wa Mkristo;
Mtume Paulo anawaandikia Warumi kwamba ni sala yake kwamba wote waokolewe, kwa maana wana juhudi katika Mungu lakini si katika maarifa. Paulo anaendelea kusema kwamba wakiwa hawaijui haki ya Mungu na wakitaka kuithibitisha haki yao, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.
Sasa katika kukosa hayo maarifa ya kuwa chini ya haki ya Mungu, Paulo ndipo anakazia kwenye mstari wa nne, kwamba Kristo ndiye mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki. Nasi tusichelewe wala kuzunguka, tumwamini Kristo ili tuhesabiwe haki. Amina
Uwe na wiki njema ukiwa huru katika Kristo Yesu.
Heri Buberwa
