Jumatano asubuhi 05.08.2026;
Ufunuo wa Yohana 2:8-11
[8]Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika;
Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai.
[9]Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.
[10]Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.
[11]Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Mwenendo wenu uwe wa hekima;
Ni ujumbe kwa Kanisa lililoko Smirna.
Yohana anafunuliwa kusema kuwa Bwana anaijua dhiki na umaskini wa Smirna. Lakini katika umaskini huo, waamini wa Smirna wanatiwa moyo pale Yohana anaposema "lakini u tajiri". Anawatia moyo kutoogopa mambo yatakayowapata, bali wawe waaminifu na Bwana atawapa taji ya uzima.
Kwa Kanisa la leo naweza kusema Bwana anaujua udhaifu wetu, na katika udhaifu huo tunatiwa nguvu tuwe imara. Hatutakiwi kuogopa maana Bwana yu pamoja nasi. Ndiyo maana anasema tuwe waaminifu, naye atatupa taji ya uzima. Basi kuwa mwaminifu katika Kristo hata kufa ili uipokee taji ya uzima. Amina
Siku njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650
