Isaya 32:1-4 - 14-08-2026

Date
Reading
Isaya 32:1-4

Ijumaa asubuhi tarehe 14.08.2026

Isaya 32:1-4
1 Tazama, mfalme atamiliki kwa haki, na wakuu watatawala kwa hukumu.
2 Na mwanadamu atakuwa kama mahali pa kujificha na upepo, na mahali pa kujisitiri na dhoruba; kama mito ya maji mahali pakavu, kama kivuli cha mwamba mkubwa katika nchi yenye uchovu.
3 Tena macho yao waonao hayatakuwa na kiwi, na masikio yao wasikiao yatasikiliza.
4 Tena moyo wa mtu mwenye hamaki utafahamu maarifa, na ndimi zao wenye kigugumizi zitakuwa tayari kunena sawasawa.

Haki huleta amani na ustawi;

Ni utabiri wa Isaya juu ya ahadi ya ufalme wenye haki kwa Israeli. Wanaahidiwa Taifa ambalo mfalme atamiliki kwa haki na wakuu watatawala kwa hukumu. Wanadamu wanaahidiwa kuwa na nchi ambayo itakuwa mahali salama, wakitakiwa kutenda kwa wema.

Mungu alikuwa anawaahidi Israeli Taifa lenye haki itokayo kwake. Ahadi hii hudumu sasa, maana hata sisi huhesabiwa haki kwa neema yake. Tunapomwamini Yesu Kristo tunafanyika wake siku zote, na kwa neema yake anatuhesabia haki. Hatuwezi kujihesabia haki! Kwa mfano huo, nasi tuwape jirani zetu haki zao ili tuwe na amani na ustawi. Amina
Siku njema

Heri Buberwa 
Mlutheri
Butainamwa/Bukoba