Date
Reading
Isaya 54:13

Jumamosi asubuhi tarehe 03.10.2026;
Isaya 54:13
Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi.
Tuwalee watoto katika njia ipasayo;
Sura ya 54 ya Kitabu cha Isaya inahusu faraja, kurejeshwa kwa Israeli na upendo wa Mungu usiokoma, baada ya unabii wa Israeli kuteseka (sura ya 53). Bwana anasimama juu ya Israeli kama mume kwa ishara ya ukuu wake kwa ahadi ya kuwatoa uhamishoni na kuwalinda siku zote. Ni ahadi ya kuwatunza watu wote, hata watoto kufundishwa na Bwana, wakiwa na amani.
Ahadi ya Bwana kuwarejesha toka uhamishoni ilihusisha hata watoto. Mungu haachi mtu, ndiyo maana juma hili tunakumbushwa juu ya kuwalea watoto katika njia iwapasayo. Somo linatoa ahadi kwa Israeli kwamba Mungu atakuwa na watoto wao pia. Tuendelee kuwaleta kwa Yesu, tukiwalea kwa msingi wa neno la Mungu ili kulijenga Kanisa lake. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
