October 2024

Matangazo ya Usharika tarehe 20 Oktoba 2024

MATANGAZO YA USHARIKA  

TAREHE 20 OKTOBA, 2024

SIKU YA BWANA YA 21 BAADA YA UTATU 

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

TUISHINDANIE IMANI KATIKA KRISTO YESU 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna .mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 13/10/2024

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

Sikukuu ya Mikaeli na Watoto 2024 | Azania Front Cathedral

Siku ya Jumapili tarehe 29 Septemba 2024 katika Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front ilifanyika Sikukuu ya Mikaeli na Watoto; Sikukuu ambayo hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kumkumbuka malaika Mikeli na watakatifu wote pamoja na watoto. Ibada hii hufanyika kwa kuongozwa na watoto wakisaidiana na walimu wao pamoja na watumishi wengine wa usharika (parish workers).