November 2023

AZF | Sikukuu ya Mavuno 2023: "Sikukuu Kamili ya Kanisa ya Utoaji" - Dean Chediel Lwiza

Siku ya Jumapili, tarehe 22/10/2023, KKKT -DMP Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral ulifanya maadhimisho ya kilele cha sikukuu ya mavuno ya mwaka 2023, maadhimisho ambayo hufanyika kila mwaka ili kutoa fursa kwa washarika kumtolea Mungu sehemu ya matunda au mavuno ya kazi walizozifanya kwa kipindi cha mwaka mzima.

Ibada ya kusherehekea sikukuu hii ya mavuno kwa mwaka huu imefanyika katika viwanja vya usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral huku ikihudhuiriwa na mamia ya washarika waliojitokeza kwa wingi wakiwa na mavuno yao tayari kwa kumtolea Mungu.