VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

Date
Reading
Yeremia 11:9-11

Ijumaa asubuhi tarehe 20.11.2026;

Yeremia 11:9-11

9 Naye Bwana akaniambia, Fitina imeonekana katika watu wa Yuda, na katika wenyeji wa Yerusalemu.

10 Wameyarudia maovu ya baba zao, waliokataa kusikia maneno yangu; wamewafuata miungu mingine na kuwatumikia; nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda, wameyavunja maagano yangu niliyoyafanya na baba zao.

11 Basi, Bwana asema hivi, Tazama, nitaleta mabaya juu yao, ambayo hawataweza kuyakimbia; nao watanililia, walakini sitawasikiliza.

Hukumu ya mwisho inakuja;
Mistari tuliyoisoma inahusu uasi wa watu wa Yuda na Yerusalemu dhidi ya Mungu wakirudia dhambi za mababu zao kwa kuabudu miungu mingine na kuvunja agano. Kutokana na ukaidi huo, Mungu anawatangazia hukumu na maafa ambayo hayawezekani kuepukika akisema hatawasikiliza watakapomlilia.
Ni ujumbe unaotutaka kutafakari njia zetu, tukatubu na kubadilika. Tuishi kwa kadri ya neno la Mungu kama tulivyoitwa, na siyo kufuata mambo ya zamani. Tubaki katika njia sahihi ambayo ni imani katika Yesu Kristo aliye njia kweli na uzima. Amina

Siku njema

Heri Buberwa 

Mlutheri