VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

Date
Reading
Warumi 8:24-25

Jumatatu asubuhi tarehe 09.11.2026;

Warumi 8:24-25

24 Kwa maana tuliokolewa kwa taraja; lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana, hakuna taraja tena. Kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho?

25 Bali tukikitarajia kitu tusichokiona, twakingojea kwa saburi.

Mwenye kuvumilia hata mwisho ataokoka;
Mtume Paulo anawaandikia watu wa Rumi kwamba waliokolewa kwa taraja. Taraja ni nini? Ni hali ya kutazamia, kutumaini, au kusubiri jambo fulani litokee au lipatikane katika siku za usoni. Kwa hiyo Paulo anamaanisha kwamba waaminio wamekwisha kuokolewa kwa imani katika Yesu Kristo, na bado wanausubiria mwisho wao ambao ni ufufuo, na uzima wa milele. 
Tunapoendelea kuungojea mwisho wetu, Paulo anatukumbusha kuwa na saburi, yaani uvumilivu. Kumbe tunaalikwa kuwa wavumilivu katika njia ya imani ili tuufikie ule mwisho mwema tulioahidiwa. Basi simama kwa imani yako, maana mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka. Amina
Uwe na wiki njema yenye uvumilivu 

Heri Buberwa