VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

Date
Reading
Waebrania 8:8-12

Jumatatu asubuhi tarehe 02.11.2026;

Waebrania 8:8-12

8 Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya;

9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana.

10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.

11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.

12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena.

Tunaitwa kuwa wenyeji wa Mbinguni;
Utangulizi;
Mwandishi wa waraka kwa Waebrania katika somo tulilosoma anamnukuu Nabii Yeremia 31:31-34 akitangaza Agano jipya ambalo liliondoa sheria ya Musa. Agano jipya lilijaa neema ya Mungu kwa wote waaminio. Angalia rejea ya mwandishi;

Yeremia 31:31-34

31 Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.

32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.

33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.

Somo lenyewe;
Mungu alibadili Agano la zamani na kuwapa watu wake Agano jipya. Agano la kale lilitawaliwa na sheria na bado watu hawakubaki katika Agano la Bwana. Mungu anatangaza Agano ambalo limejaa neema, ambalo lina hakika ya msamaha wa dhambi mara mtu anapotubu. 
Wakati tuliomo ni wa neema ambapo ahadi ya Mungu ni kutuokoa kwa neema, yaani tunaishi kwa neema ya Mungu ambaye ahadi zake hutimia kwetu. Katika ahadi zake, kila mmoja anayo nafasi ya kumwendea wakati wowote kwa imani na kumweleza haja zake, tofauti na watu wa kale waliopitia kwa Kuhani. Kumbe Kristo yuko kwa kila mmoja. Basi tumia nafasi hiyo ya kuwa na Kristo ili uwe mwenyeji wa mbinguni. Amina

Uwe na wiki njema

Heri Buberwa Nteboya 

 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com