Ruthu 2:14-18 - 16-07-2026

Date
Reading
Ruthu 2:14-18

Alhamisi asubuhi tarehe 16.07.2026

Ruthu 2:14-18

[14]Tena wakati wa chakula huyo Boazi akamwambia, Karibu kwetu, ule katika mkate wetu, na ulichovye tonge lako katika siki yetu. Basi akaketi pamoja na wavunaji, nao wakampitishia bisi, naye akala akashiba, hata akasaza.

[15]Naye alipoinuka tena ili aende kuokota masazo, huyo Boazi aliwaagiza vijana wake akisema, Mwacheni aokote hata kati ya miganda, wala msimkemee.

[16]Tena mtoleeni kidogo katika matita na kukiacha, na akiokote, wala msimkataze.

[17]Basi Ruthu akaokota masazo kondeni hata jioni; kisha akazipura zile nafaka alizoziokota, zikawa yapata efa moja ya shayiri.

[18]Akajitwika, akaenda zake mjini. Akamwonyesha mkwewe zile alizoziokota; akavitoa vile vyakula alivyovisaza alipokwisha kushiba, akampa.

Upendo waMungunautawale;

Tunaendelea na habari ya Ruthu akiwa kwa Boazi. Asubuhi hii tunaona Boazi akimkaribisha Ruthu kwa chakula, na baada ya kula anamruhusu kubeba chakula kilichobaki.

Boazi kumkaribisha Ruthu chakula ni ishara ya upendo, ni tendo la huruma. Huu ni ujumbe kwetu asubuhi ya leo, kwamba tusisahau kufanya  matendo ya huruma. Kwa njia hiyo  tunamwakilisha Yesu mwenye huruma ya kweli. Amina

Siku njema

Heri Buberwa