VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

Date
Reading
Marko 5:21-24

Alhamisi asubuhi 24.09.2026;

Marko 5:21-24

21 Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng'ambo katika kile chombo, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari.

22 Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake,

23 akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yu katika kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi.

24 Akaenda pamoja naye; mkutano mkuu wakamfuata, wakimsonga-songa.

Mungu amejaa huruma;
Asubuhi ya leo tunamsoma mtu mmoja katika wakuu wa Sinagogi aliyeitwa Yairo, alimfuata Yesu akaanguka miguuni pake akimsihi sana na kusema Binti yangu mdogo yu katika kufa. Alimuomba Yesu aweke mkono juu yake apone na kuendelea kuishi. Yesu alikubali akaenda pamoja naye, mkutano wakimfuata.
Baada ya Yairo kumuomba Yesu amponye binti yake, tunaona Yesu alikubali na kuondoka na Yairo. Yesu alionesha kumhurumia Yairo na kuondoka naye. Hata sisi leo tukiomba Yesu husikia sala  na kutupa haja zetu kwa huruma yake. Tumwamini yeye daima. Amina

Siku njema

Heri Buberwa