Luka 10:25-28 - 17-07-2026

Date
Reading
Luka 10:25-28

Ijumaa asubuhi tarehe 17.07.2026;

Luka 10:25-28

25 Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?

26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?

27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.

28 Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.

Upendo wa Mungu na utawale;

Mwanasheri anamjaribu Yesu akiuliza kuwa afanye nini ili aurithi uzima wa milele, na Yesu bila kusita anamuuliza torati inasemaje? Yule ndugu anajibu kwa kuinukuu torati aliyoijua, kwamba ni kwa kumpenda Mungu kwa moyo wote, roho, nguvu na akili. Hakusahau kumpenda jirani pia.

Huyu mwanasheria aliuliza kitu alichokijua, maana alikuwa anamjaribu Yesu. Alichotakiwa ni kuitunza amri ya upendo kwa imani katika Kristo, pasipo sheria. Sisi amri kuu tunaijua, basi tusiishi kwa maswali kuhusu hilo wala wasiwasi. Tuwe na upendo wa Kristo miongoni mwetu. Kama Yesu alivyomwambia yule ndugu, "tufanye hivyo nasi tutaishi", yaani tupendane katika Kristo aliyetuita. Amina

Ijumaa njema

Heri Buberwa