VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

Date
Reading
Kutoka 20:12

Jumanne asubuhi tarehe 29.09.2026;

Kutoka 20:12

Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

Tuwalee watoto katika njia ipasayo;
Ni ujumbe wa kuwaheshimu baba na mama kama Mtume Paulo alivyourejea katika waraka tuliousoma Jumapili kutoka kwa Waefeso sura ya 6. Tuliona kwamba kuheshimu ni kusikiliza na kufuata, ni jambo la muda wote, yaani heshima ni ya kudumu. 
Kuheshimu wazazi siyo kwa watoto wadogo tu, ni kwa waamini wote. Kila mmoja anatakiwa kuwaheshimu wazazi wake. Hata kama wazazi (au mzazi) hawapo, waheshimu waliobaki kama wazazi wako. Kuwaheshimu wazazi ni agizo toka kwa Mungu. Amina

Siku njema

Heri Buberwa