Ezekiel 33:10-12 - 28-07-2026

Date
Reading
Ezekiel 33:10-12

Jumanne jioni tarehe 28.07.2026;

Ezekieli 33:10-12

10 Na wewe, mwanadamu, sema na nyumba ya Israeli; Ninyi mwasema hivi, kwamba, Makosa yetu na dhambi zetu ni juu yetu, nasi tumedhoofika katika dhambi hizo; basi tungewezaje kuwa hai?

11 Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?

12 Na wewe, mwanadamu, waambie wana wa watu wako, Haki yake mwenye haki haitamwokoa, katika siku ya kukosa kwake; na kwa habari ya uovu wake mtu mwovu, hataanguka kwa ajili ya uovu huo, siku ile atakapoghairi na kuuacha uovu wake; wala yeye aliye mwenye haki hataweza kuishi kwa haki yake, siku ile atakapotenda dhambi.

Mungu hupendezwa na moyo wa toba;

Baada ya Nabii Ezekieli kuwaambia Israeli kuacha njia mbaya ili wasife katika uovu kama tulivyoona jana jioni, Israeli walijiona dhambi zao kuwa juu yao, wakiwa wamedhoofika katika dhambi hizo na kujiuliza wangewezaje kuwa hai? Ndipo Bwana anamtuma Ezekieli kuwaambia kwamba hafurahii kufa kwa mtu mwovu, sasa walitaka kufa?

Ujumbe huu unatujia usiku huu, kwamba Yesu Kristo hafurahii sisi kama watoto wake kufa dhambini. Tujiulize, tunataka kufa dhambini? Tukumbushane kuishi maisha ya toba maana Mungu hupendezwa na moyo wa toba. Amina

Usiku mwema

Heri Buberwa