Date
Reading
Zaburi 96:7-8

Jumamosi asubuhi tarehe 12.09.2026;
Zaburi 96:7-8
7 Mpeni Bwana, enyi jamaa za watu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu.
8 Mpeni Bwana utukufu wa jina lake, Leteni sadaka mkaziingie nyua zake.
Tutende wajibu wetu kwa Mungu kwa uaminifu;
Zaburi ya 96 inahusu sifa kwa Mungu atoaye hukumu. Ni wito wa kumpa Bwana Utukufu na nguvu hekaluni mwake. Mwimbaji wa zaburi hii anawaita watu kumsifu Mungu na kuleta sadaka nyumbani mwa Bwana.
Sadaka inayoletwa nyumbani mwa Bwana lazima itokane na kazi za mikono ya waaminio. Kwa hiyo ujumbe unatutaka kufanya kazi na kumtolea Bwana kwa ajili ya kazi yake. Itikio la wokovu wetu ni uwajibikaji wetu na kuitenda kazi ya Mungu kwa uaminifu. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
