Yeremia 6:11-15 - 10-09-2026

Date
Reading
Yeremia 6:11-15

Alhamisi asubuhi tarehe 10.09.2026

Yeremia 6:11-15

11 Lakini nimejaa ghadhabu ya Bwana; nimechoka kwa kujizuia; imwageni juu ya watoto walio njiani, na juu ya kusanyiko la vijana pia; maana hata mume atatwaliwa pamoja na mkewe, mzee pamoja na yeye aliyetimiza siku zake.

12 Na nyumba zao zitakuwa mali za watu wengine, mashamba yao na wake zao pamoja; kwa kuwa nitaunyosha mkono wangu juu ya wenyeji wa nchi hii, asema Bwana.

13 Kwa maana, tangu aliye mdogo hata aliye mkubwa miongoni mwao, kila mmoja ni mtamanifu; na, tangu nabii hata kuhani, kila mmoja hutenda mambo ya udanganyifu.

14 Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.

15 Je! Walitahayarika, walipokuwa wameunda machukizo? La, hawakutahayarika hata kidogo, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi, wataanguka miongoni mwa hao waangukao; wakati nitakapowajilia wataangushwa chini, asema Bwana.

Tutende wajibu wetu kwa Mungu kwa uaminifu;
Ujumbe tuliousoma ni maonyo ya unabii wa kuharibiwa kwa Yerusalemu na majeshi yasiyo na huruma toka Yerusalemu ya Kaskazini (Babeli) kwa sababu ya dhambi, uchoyo, mioyo migumu n.k. Somo linaonesha Bwana kujaa ghadhabu na kuwaadhibu watu walioacha kumcha. Watu wanaonekana kuachwa na mali zao kutwaliwa! 
Kwa hiyo Israeli wanapewa taarifa ya kuvamiwa na kuharibiwa kwa nchi yao! Na sababu inatajwa, kuendekeza vitendo viovu. Kwa tafakari ya juma hili, naweza kusema wanapewa taarifa ya kuangamizwa kwa sababu ya wao kutotimiza wajibu wao kwa Mungu. Mafanikio yetu yanategemea bidii yetu katika kazi kwa kumtanguliza Mungu atupaye nguvu kumtumikia. Amina

Siku njema

Heri Buberwa