Date
Reading
Warumi 9:30-33
Jumamosi asubuhi tarehe 31.10.2026;
Warumi 9:30-33
30 Tuseme nini, basi? Ya kwamba watu wa Mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani;
31 bali Israeli wakiifuata sheria ya haki hawakuifikilia ile sheria.
32 Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuifuata kwa njia ya imani, bali kana kwamba kwa njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile likwazalo,
33 kama ilivyoandikwa, Tazama, naweka katika Sayuni jiwe likwazalo, na mwamba uangushao; Na kila amwaminiye hatatahayarika.
Mwenye haki ataishi kwa imani;
Watu wa mataifa, yaani wasio Wayahudi hawakuifuata sheria ya Mungu, lakini waliposikia Injili ya Yesu Kristo waliipokea kwa imani na kuhesabiwa haki bure. Israeli walijitahidi sana kuifuata sheria ya Musa ili kupata haki mbele za Mungu, lakini hawakufanikiwa kwa sababu walitegemea matendo yao wenyewe badala ya kuweka imani yao kwa Yesu.
Kwa mujibu wa Paulo, Kristo mwenyewe ndiye jiwe likwazalo kwa wale wanaotaka kujiokoa kwa matendo yao. Badala ya kumtegemea yeye, walijikwaa kwake. Paulo anahitimisha kwa kusema kuwa wale wote wamwaminio Yesu ambaye ni jiwe la thamani hawataaibika kamwe. Kumbe sheria haina nafasi, bali imani katika Kristo Yesu. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
