Jumanne asubuhi tarehe 04.08.2026
Waefeso 4:17-19
17 Basi nasema neno hili, tena nashuhudia katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao;
18 ambao; akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao;
19 ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani.
Mwenendo wenu uwe wa hekima;
Mtume Paulo anawaandikia waamini wa Kanisa la Efeso kuacha maisha ya zamani na kuishi maisha mapya katika Kristo Yesu. Anawaambia wasienende kama mataifa waenendavyo katika ubatili wa nia zao. Anasema hao mataifa akili zao zimetiwa giza, wameiacha njia ya kweli kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, na kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao.
Mtume Paulo anapoandika kutoenenda kama mataifa waenendavyo, anatukumbusha kuacha maisha ya zamani, yaani maisha ya kutokumuamini Yesu. Anatukumbusha kumshika Kristo na ahadi zake, yaani tusiiache imani. Hii ndiyo hekima muhimu kuliko zote, yaani kudumu katika imani katika Kristo Yesu. Amina
Jumanne njema
Heri Buberwa
