Jumatano asubuhi tarehe 29.07.2026;
Waebrania 12:5-11
5 Tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye;
6 Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye.
7 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?
8 Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.
9 Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?
10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.
11 Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.
Mungu hupendezwa na moyo wa toba;
Mwandishi wa waraka kwa Waebrania anarejea Mithali za Suleimani kwa wasomaji wake kwamba wasiyasahau maonyo ya kutoyadharau mausia ya Bwana, wala wasizimie moyo wakikemewa naye maana Bwana humrudi na kumpiga kila mwana amkubaliye. Nasema hivi kwa sababu naona rejea hii hapa;
Mithali 3:11-12
11 Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na Bwana, Wala usione ni taabu kurudiwa naye.
12 Kwa kuwa Bwana ampendaye humrudi, Kama vile baba mwanawe ampendezaye.
Mwandishi anaendelea kurejea historia jinsi Baba zao walivyowarudi, nao wakawastahi. Anasema hao walikuwa baba zao wa mwili waliowarudi wakawastahi, sasa iweje wasiwe watii kwa Kristo? Anasema baba zao walipowarudi ilikuwa kwa faida yao. Tukitubu dhambi ni kwa faida yetu. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
