VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

Date
Reading
Mathayo 4:23-25

Jumanne asubuhi tarehe 22.09.2026;

Mathayo 4:23-25

23 Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu.

24 Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.

25 Na makutano mengi wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Uyahudi, na ng'ambo ya Yordani

Mungu amejaa huruma;
Yesu baada ya kuwateua wanafunzi wa kwanza anaendelea na kazi yake akifundisha na kuhubiri habari njema za ufalme wa Mungu. Aliponya magonjwa na udhaifu wa kila namna. Habari zilienea, wakaletwa waliokuwa hawawezi, wenye maradhi mbalimbali na mateso, pepo, kifafa, kupooza na wengine wengi wakapona
Tunachoona ni huduma ya Yesu iliyoambatana na matendo ya huruma. Hakuhubiri Injili na kufundisha tu, bali kama tulivyoona kwenye somo aliwaponya wengi. Ni kwa huruma yake hiyo hiyo  ametuokoa, akituita kuishi kwa huruma kama yeye. Kuwa na huruma kama Kristo alivyo na huruma.Amina

Siku njema

Heri Buberwa