Matangazo ya usharika ya tarehe 20 Septemba 2026

DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI MATANGAZO YA USHARIKA  TAREHE 20 SEPTEMBA, 2026

SIKU YA BWANA YA 16 BAADA YA UTATU NENO LINALOTUONGOZA NI:

MUNGU AMEJAA HURUMA”

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 13/09/2026

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

- Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONTCATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 13/09/2026 ni Washarika 759 na Sunday School  262

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=

7. Jumapili ijayo tarehe 27.09.2026 ni Sikukuu ya Mikaeli na watoto,  hivyo ibada zote zitaongozwa na watoto. Aidha Jumamosi Mikaeli ya kwanza ratiba itaanza saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 Alasiri.

8. Kwaya ya Umoja inaendelea na mazoezi ya Reformation kila Jumanne na Jumatano  saa 11:00 jioni. Wanakwaya wote mnaombwa kuhudhuria bila kukosa na kwa wakati.

9. Vitabu vya Ibada ya nyumba kwa nyumba vinapatikana  dukani.

10. Shukrani

Familia ya marehemu Mzee Mathew Munisi itamtolea Mungu sadaka ya shukrani jumapili ijayo ya tarehe 27.09.2026 katika ibada ya kwanza wakimshukuru Mungu kwa jinsi alivyowasimamia wakati wa msiba wa mpendwa wao.

Neno kutoka Zaburi 46 na wimbo namba 317  Chakutumaini sina.

Familia ya marehemu Mama Hilda Kapimo Lwezaula itamtolea Mungu sadaka ya shukrani leo katika ibada ya kwanza wakimshukuru Mungu kwa jinsi alivyowasimamia wakati wa msiba wa mpendwa wao.

Neno kutoka Wafilipi 4:6-7 na wimbo kutoka Kwaya ya Upendo.

11. NDOA. Ndoa za Washarika

Hakuna ndoa ya Msharika

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Mjini kati: Itafanyika Kanisani siku ya Jumamosi saa 1:00 kamili asubuhi.

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo Kwa.MAMA KOROSO

- Kinondoni: kwa: DR ONESMO

- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa DADA DOSCAR

- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: kwa Bw &Bibi Zebadia Moshi

13. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya azaniafront.or.tz, pia tuna kurasa Facebook na Instagram.

14. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki