
Jumatatu asubuhi tarehe 28.09.2026
Marko 9:33-37
33 Wakafika Kapernaumu; hata alipokuwamo nyumbani, akawauliza, Mlishindania nini njiani?
34 Wakanyamaza; kwa maana njiani walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa.
35 Akaketi chini, akawaita wale Thenashara akawaambia, Mtu atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote.
36 Akatwaa kitoto, akamweka katikati yao, akamkumbatia, akawaambia,
37 Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.
Tuwalee watoto katika njia ipasayo;
Yesu alitabiri kufa na kufufuka kwake, wanafunzi wake hawakuelewa, wakaogopa hata kumuuliza. Ndipo wakaanza kuulizana kwamba nani kati yao angekuwa mkubwa. Yesu akawaambia kuwa atakaye kuwa mkubwa awe mtumishi wa wote. Akamuweka kitoto katikati yao na kuwaambia kuwa ampokeaye mtoto ampokea Kristo.
Kwenye Injili ya Mathayo Yesu anasema anyenyekeaye kama mtoto afaa kuwa kiongozi;
Mathayo 18:2-4
2 Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,
3 akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
4 Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.
