VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

Date
Reading
Isaya 29:17-24

Alhamisi asubuhi tarehe 12.11.2026;

Isaya 29:17-24

17 Je! Si muda mdogo uliobaki, na Lebanoni itageuzwa kuwa shamba lizaalo sana, na lile shamba lizaalo sana litahesabiwa kuwa msitu?

18 Na katika siku hiyo viziwi watasikia maneno ya hicho chuo, na macho ya vipofu yataona katika upofu na katika giza.

19 Wanyenyekevu nao wataongeza furaha yao katika Bwana, na maskini katika wanadamu watafurahi katika Mtakatifu wa Israeli.

20 Kwa maana mwenye kutisha ameangamizwa, naye mwenye dharau amekoma, nao wote watazamiao uovu wamekatiliwa mbali;

21 hao wamfanyao mtu kuwa amekosa katika neno, na kumtegea mtego yeye aonyaye langoni, na kumgeuza mwenye haki kwa kitu kisichofaa.

22 Basi, Bwana aliyemkomboa Ibrahimu asema hivi, katika habari za nyumba ya Yakobo; Yakobo hatatahayarika sasa, wala uso wake hautabadilika rangi yake.

23 Bali atakapowaona watoto wake, walio kazi ya mikono yangu, katikati yake, wao watalitakasa jina langu; naam, watamtakasa Mtakatifu wa Yakobo, nao watamcha Mungu wa Israeli.

24 Hao nao wakosao rohoni mwao watapata kufahamu, na hao wanung'unikao watajifunza elimu.

Mwenye kuvumilia hata mwisho ataokoka;
Isaya anatoa unabii unaohusu ukombozi wa nyumba ya Israeli. Anaanza kwa kuuliza kuwa muda mdogo uliobaki Lebanoni itageuzwa shamba lizaalo sana? na lile shamba lizaalo sana litahesabiwa kuwa msitu? Anaongelea hali ya vipofu na viziwi siku hizo, wanyenyekevu na maskini kufurahi katika Mtakatifu Israeli. 
Isaya anaendelea kutabiri mwenye kutisha kuangamizwa,  mwenye dharau kukoma,na watazamiao uovu kukataliwa mbali. Isaya anatoa uhakika wa kila aliyeko katika nyumba ya Yakobo kutotahayarika. Wote walio katika Bwana na wakosao rohoni watapata kufahamu, na hao wanung'unikao watajifunza elimu.
Israeli walikuwa na tishio la kupelekwa uhamishoni, lakini unabii wa Isaya unaonesha Bwana kutowaacha watu wake. Ahadi ya Mungu kuwa nasi inadumu hata sasa, kwamba katika hali yoyote Bwana yuko nasi, hatuachi. Tuendele kuvumilia katika yeye ambaye hatuachi ili tuufikie mwisho mwema aliotuahidi. Amina

Siku njema

Heri Buberwa 

Mlutheri