VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

Date
Reading
Danieli 12:5-13

Jumanne asubuhi tarehe 10.11.2026;

Danieli 12:5-13

5 Ndipo mimi, Danielii, nikatazama, na kumbe, wamesimama wengine wawili, mmoja ukingoni mwa mto upande huu, na mmoja ukingoni mwa mto upande wa pili.

6 Na mmoja akamwuliza yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, Je! Itakuwa muda wa miaka mingapi hata mwisho wa mambo haya ya ajabu?

7 Nami nikamsikia yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, hapo alipoinua mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni; akaapa kwa yeye aliye hai milele na milele, ya kwamba itakuwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati; tena watakapokuwa wamekwisha kuvunja nguvu za hao watu watakatifu, ndipo mambo hayo yote yatakapotimizwa.

8 Nami nikasikia, lakini sikuelewa; ndipo nikasema, Ee Bwana wangu, mwisho wa mambo haya utakuwaje?

9 Akasema, Enenda zako, Danielii; maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho.

10 Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.

11 Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na tisini.

12 Heri angojaye, na kuzifikilia siku hizo elfu na mia tatu na thelathini na tano.

13 Lakini enenda zako hata utakapokuwa mwisho ule; maana wewe utastarehe, nawe utasimama katika kura yako mwisho wa siku hizo.

Mwenye kuvumilia hata mwisho ataokoka;
Somo la asubuhi hii ni hitimisho la unabii wa Danieli ambaye anaona watu wawili waliosimama kando ya mto, na mwingine upande wa pili. Wanaulizana mwisho wa kuona mambo ya ajabu, mmoja anatoa hesabu ambayo ni miaka mitatu na nusu (7). Danieli hakuelewa, alipomuuliza Bwana akaambiwa kuondoka maana mambo yatadhihirika wakati wa mwisho.
Danieli anaendelea kuoneshwa kwamba wengi watajitakasa na kujifanya weupe, bali wabaya watatenda mabaya, lakini wenye hekima wataelewa. Zinatajwa maelfu ya siku tangu sadaka ya kuteketezwa itakapoondolewa, ikiwa heri kwa angojaye na kuzifikia hizo siku. Lakini Danieli anahakikishiwa kwenda kwa amani, maana yeye atastarehe katika siku hizo.
Tunajifunza nini;
1. Mateso ni ya muda tu - Linapotokea swali kwamba mambo haya (mateso) yataisha lini, yule mtu aliyevaa nguo za kitani anataja muda ambao ni miaka mitatu na nusu. Funzo la msingi hapa ni kuwa mateso hayadumu kwa waaminio. 
2. Majaribu huwakomaza waaminio kuliko kuwaharibu - Somo linaonesha katikati ya mateso wengi watajitakasa na kusafika. Upo uhakika wa kuufikia mwisho mwema tusipomuacha Kristo hata katika majaribu.
3. Somo linataja siku kwa idadi (1,290 na 1,335) na kutangaza baraka kwa wote wangojeao na kuzifikia siku hizo. Idadi ya siku hizo inatukumbusha kuwa wavumilivu katika Bwana ndipo tutaokoka. Amina

Siku njema

Heri Buberwa 

Mlutheri