%AutoEntityLabel: 98ff23ea-f376-4079-a9ea-0540f67162cb%

Date
Reading
1 Petro 5:5-7

Jumatano asubuhi 19.08.2026

1 Petro 5:5-7
5 Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.
6 Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;
7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

Mungu huwainua wanyenyekevu;

Petro analiandikia Kanisa yahusuyo kulichunga kundi la Mungu, na uwajibikaji kwa kila aaminiye. Sehemu tuliyosoma anawasihi vijana kuwatii wazee, halafu Kanisa zima kujifunga unyenyekevu ili wapate kuhudumiana maana Mungu huwapinga wenye kiburi na kuwapa wanyenyekevu neema.

Petro anasisitiza kunyenyekea kwa Mungu na kumtegemea yeye pekee, maana hujishughulisha na mambo yetu. Ni wito unaotutaka kuishi maisha ya unyenyekevu tukimtegemea Kristo pekee, maana ndiye mwenye hatma yetu. Amina
Siku njema

Heri Buberwa 
Mlutheri